Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wanachama wa Kikundi cha Ufundi
wa vyombo vya Moto cha Wagodo Gereji cha Wete Pemba hapo katika
Ukumbi wa Hoteli ya Hifadhi Tibirinzi Chake chake Pemba.
Balozi Seif akimkabidhi Fundi Mkuu
wa Wadogo Gereji Bwana Hussein Moh’d Said Zana za Ufundi
akitekeleza ahadi aliyowapa wanachama wa kikundi hicho cha ufundi
zitakazowasaidia katikia harakati zao za kujitafutia mapato. (Picha
na –OMPR – ZNZ).
Press Release:-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi amesema licha ya Serikali kujitahidi kutafua
mbinu za kukabiliana na tatizo la ajira lakini wananchi wenyewe hasa
Vijana waliomaliza masomo yao wana fursa na wajibu wa kuunda vikundi
vya ujasiriamali vitakavyoweza kusaidia kukabiliana na tatizo hilo.
Alisema suala la ajira hivi sasa
limekuwa changamoto kubwa inayoikabili Dunia ambapo hata Mataifa
yaliyoendelea kiuchumi yanaguswa na changamoto hiyo inayoweza
kupungua iwapo jitihada kati ya Serikali ya taasisi Binafsi
zitashirikiana katika kuunganisha nguvu za pamoja.
Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo
wakati akikabidhi zana za Kiufundi { Tools Box } kwa Kikundi cha
Vijana wajasiri amali cha Wadogo Garage hapo Hoteli ya Hifadhi
Tibirinzi Mjini Chake chake kufuatia ziara yake ya hivi karibuni
aliyoifanya Kisiwani Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
alikuwa akitekeleza ahadi aliyowapa Vijana hao wenye mastakimu yao
katika Mtaa wa Wete mkabala ya Jengo la Posta ambao
wanaojishughulisha na shughuli za ufundi wa Magari, Vespa, Piki piki
pamoja na Mashine zinazotumia umeme.
Alisema juhudi mbali mbali
zitachukuliwa na Serikali Kuu katika kuona vijana hao wanapata zana
kamili zitakazokidhi mahitaji yao ya kiufundi na kuwataka kuhakikisha
kwamba wateja wanaowahudumia wanalipa fedha za matengenezo kutokana
na vyombo wanavyopeleka ili fedha zinazokusanya zisasaidie
kuendesha maisha yao ya kila siku.
Aliwapongeza vijana hao wa Kikundi
cha ufundi cha Wadogo Gereji kwa uamuzi wao wa kujikusanya pamoja na
kuanzisha miradi itakayotowa mwanga katika kukabiliana na ukali wa
maisha hapo baadaye.
Balozi Seif amekuwa akisisitiza
kwamba Serikali imeanzisha mfuko wa Uwezeshaji kupitia Wizara ya
Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana Wanawake na Watoto ambao umelenga
kuwasaidia wananchi waliojikusanya pamoja kwa kupatiwa mikopo ya
kuendesha miradi yao ya Kiuchumi.
Nao Vijana hao wa Wadogo Gereji
Wete Pemba walimshukuru na kumpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif kwa jitihada zake anazoendelea kuzichukuwa kila
kukicha katika kujaribu kusaidia kuunga mkono jitihada za wananachi
mbali mbali walioamua kujiletea maendeleo kupitia vikundi vya
wajasiri amali.
Walisema juhudi za Balozi Seif ziko
wazi na kushuhudiwa na Wananchi waliowengi Nchini na zinapaswa
kuungwa mkono sambamba na kuigwa na Viongozi wengine wa Taasisi za
umma na hata zile za kiraia zinazotoa huduma za maendeleo na kiuchumi
hjapa Nchini.
Wakizungumzia changamoto
wanazopambana nazo vijana hao wa Wadogo Gereji walisema kuwa ni
pamoja na ukosefu wa sehemu maalum ya kufanyia shughuli zao za
kiufundi, umuhali walionao kwa wateja wao pamoja na ukosefu wa fursa
za masomo kwa nia ya kuongeza ujuzi waliokuwa nao.
Kikundi cha wajasiri amali cha
Wadogo Gereji kilichoanzishwa miaka kadhaa iliyopita Chini ya Fundi
Mkuu Nd. Hussein Moh’d Said kikiwa na wanachama 29 hivi sasa
tayari kimeshafungua Tawi jengine la Kiufundi katika Kijiji cha
Tumbe.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni