Jumamosi, 21 Machi 2015
KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI, ZANZIBAR
Mwakilishi wa Jimbo la Mkwajuni Mhe Mbarouk Wadi Mtando akisoma baadhi ya Ibara ya Kitiba iliopendekezwa na Bunge la Katiba huku Mwanasheria Mkuu wa Serekali Mhe Said Hassan Said (katikati) na Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Ndg Asaa Rashid wakimsikiliza akisoma Ibara hizo za Katiba wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa Baraza baada ya kuhairishwa kwa mapumziko ya mchana. Kura ya Maoni ya Katiba iliopendekezwa inatarajiwa kupigiwa kura mwishoni mwa mwezi wa April2015.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wakijadiliana jambo, kushoto Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Mhe Issa Gavu, akiwa na Mhe Hijja Hassan Hijja mwakilishi wa Kiwani.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Abubakary Khamis, akiwa na Watendaji wa Wizara yake nje ya ukumbi wa baraza wakijadiliana baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho kuchangia mswada uliowakilishwa na wizara yake kwa wajumbe wa Baraza.
Mwakilishi wa Kitope Mhe Makame Mshimba akimsikiliza Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mhe Issa Gavu akizungumzia jambo na kusisitiza wakiwa nje ukumbi wa mkutano.
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Zanzibar Mhe Ismail Jussa akiwonesha Wajumbe wa Baraza Katiba Mpya iliopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba, akiwa nje ya jengo la Baraza la Wawakilishi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni