Vijana machachari wanaonolewa na kocha mwenye midadi na mkorofi Diego Simeone, timu ya soka ya Atletico Madrid imetinga hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati, Bayer Leverkusen toka Ujerumani katika mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Vicente Calderon.
Wakicheza katika kiwango cha hali ya juu mbele ya mashabiki wao waliokuwa wakiwashangilia bila kuchoka, Atletico walipambana na kumaliza dakika 120 wakiwa wamewafunga wageni wao bao 1-0.
Hata hivyo bao hilo halikutosha kuwavusha hatua ya robo fainali, kwani katika mchezo wa awali timu hiyo nayo ilifungwa bao 1-0 na Bayer Leverkusen.
Kwa matokeo, ndipo mshindi alipoamuliwa kwa mikwaju ya penati, ambapo Atletico Madrid walishinda penati 3 dhidi ya 2 za Leverkusen.
Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Fernando Torres akimpongeza mlinda mlango wao, Jan Oblak ambaye alikuwa shujaa wao katika mikwaju ya penati akitokea benchi.
Mlinda mlango wa Bayer Leverkusen akijaribu kudaka mpira wa penati uliopigwa kiufundi na Fernando Torres bila mafanikio.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni