Aliyekuwa msanii mahiri wa muziki wa
nchini Uganda, marehemu Emmanuela Mayanja Hammertone maarufu zaidi
kama AK47, anazikwa leo jioni huko Mityana katika msiba ambao
unatarajiwa kuhudhuriwa na umati mkubwa wa waombolezaji.
Maziko haya yanafuatia shughuli
kutoa heshima za mwisho kwa marehemu katika eneo la National Theatre
siku ya juzi na pia ibada ya kumsalia marehemu iliyofanyika jana
katika kanisa la Katoliki la St. Joseph huko Lweza.
Wakati huo huo polisi bado
wanaendelea na uchunguzi wa mazingira ya kifo cha marehemu,wakiwa sasa wanamtafuta mfanyausafi
wa baa ya Dejavu, Milton Mumbere kutoa maelezo akiwa kama mtu wa
mwisho kumuona marehemu katika dakika za mwisho za uhai wake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni