.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 2 Machi 2015

RAIS WA NAMIBIA HIFIKEPUNYE POHAMBA ASHINDA TUZO YA MO IBRAHIM

Rais wa Namibia anayeondoka madarakani Hifikepunye Pohamba ameshinda tuzo yenye thamani kubwa ya Mo Ibrahim inayotolewa kwa viongozi wa bara la Afrika.

Tuzo hiyo ya dola milioni 5, hutolewa kila mwaka kwa kiongozi wa nchi wa kuchaguliwa aliyeongoza vyema taifa lake na kuboresha masha ya watu wake na kisha kuondoka madarakani.

Hata hivyo tuzo za miaka iliyopita kwa mara nne katika kipindi cha miaka mitano zilishindwa kupata mshindi.

Bw. Pohamba, ambaye alikuwa ni muasi aliyepigania uhuru wa nchi yake, ametumikia taifa lake katika nafasi ya urais kwa vipindi vya mihula miwili.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni