Rais wa Vanuatu ameviambia vyombo
vya habari kuwa wananchi wake wengi wamejikuta wakiwa hawana makazi
baada ya kukumbwa na kimbunga kilichosambaratisha hali ya maisha
katika taifa hilo la kisiwa cha Pacific hapo jana.
Akiongea akiwa nchini Japana rais
huyo Baldwin Lonsdale amesema kimbunga Pam kimeharibu nyumba karibu
zote katika mji mkuu wa taifa hilo wa Port Vila, yakiwemo majengo ya
shule na zahanati.
Hali ya tahadhari imetanzazwa katika
taifa hilo dogo lenye watu 267,00 wanaoishi kwenye visiwa vipatavyo
65, ambapo hadi sasa watu nane wameripotiwa kufa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni