.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 16 Machi 2015

SAUDI ARABIA ITADAI HAKI YA KURUTUBISHA NYUKLIA IWAPO IRAN ITAACHIWA

Mmoja wa mwanafamilia mwandamizi wa familia ya Saudi Arabia ameonya programu ya nyuklia ya Iran itachangia mataifa ya ukanda huo nayo kuanzisha urutubishaji wa mafuta ya atomic.

Prince Turki al-Faisal amesema Saudi Arabia nayo pia itaomba haki kama ya Iran ya programu ya nyuklia kama ilivyo kwa mataifa mengine.

Mataifa sita dunia yanafanya mazungumzo yenye lengo la kufikia makubaliano ya kudhibiti programu ya Iran ya kurutubisha nishati ya nyuklia lakini si kusitisha kabisa.

Wakosoaji wa mambo wameonya kuwa makubaliano hayo yanaweza yakachochea ushindani wa kuwa na nishati ya nyuklia katika ukanda huo kutokana na uhasama uliopo baina ya Saudi na Iran.
 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni