SERIKALI ya Tanzania imesaini mkataba wa ukarabati wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa (KIA) wa majengo na uwanja huo na kampuni ya ujenzi ya ujenzi ya kimataifa ya Uholanzi iliyoshinda tenda ya kufanya kazi hiyo ndani ya miezi 23.
Mkataba huo umesaini na Meneja wa
kampuni hiyo, Erick Van Zuthem na mwenzake Harko Kloeze ambaye ni
mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Afrika na Afrika ya Kati, upande
wa Tanzania mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CADCO na
Mhandisi Christopher Mkoma ambaye ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na
ufundi wa uwanja huo.
Akizungumza mara baada ya kusainiwa
kwa mkataba huo, Mkurugenzi wa uendeshaji na ufundi wa uwanja huo,
Mhandisi Christopher Mkoma amesema kuwa, wanatarajia kutumia Euro
milioni 37 ambazo sawa na fedha zakitanzania Zaidi ya shilingi
bilioni 70.
Amesema katika ukarabati huo
ulioanza mara moja baada ya kusaini mkatana huo watahakikisha
unafanyika kwa wakati uliopangwa na bila kuharibu safari za Ndege.
Mkoma amesema Uwanja huo ulijengwa
na Mwalimu tangu mwaka 1971 tangu wakati huo hadi leo haujawahi
kukarabatiwa tena, hivyo uahitaji matengenezo makubwa ambayo
yaatakwenda sambamba na kuongeza miundo mbinu ya maji safi na salama
ili yaweze kuwa ya uhakika na mengi kulingana na mahitaji ya uwanja
huo.
Amesema maji yanahitajika sana kwa
sababu mbalimbali ikiwemo na kuhakikisha magari ya zimamoto hayakosi
maji kwa usalama wandee zinazotua na kuruka hapo.
Amesema kwa siku ndege 12 za
kimatifa zinatua mbali ya ndege za kawaida, hivyo vema uwanja huo
ukaaboreshwa Zaidi ili kuvutia uwekezaji na wageni wengi.
Fedha hizo zimetolewa na serikali ya
Tanzania na serikali ya Uholanzi, ili kuufanya uwanja huo unakuwa wa
kisasa Zaidi ya sasa.
Mwisho
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni