Maafisa wameeleza kuwa rubani mwenza
wa ndege ya shirika la Germanwings iliyoanguka kwenye Mlima Alps,
aliyejulikana kama Andreas Lubitz, inawezeka alikuwa anataka
kuiteketeza ndege hiyo.
Mwendesha mashtaka wa Marseille,
Brice Robin, kwa kutumia sauti zilizorekodiwa na sanduku la kurekodi
taarifa la "black box", amesema rubani huyo alikuwa
akiongoza ndege peke yake.
Amesema kuwa rubani huyo aliishusha
ndege chini kwa makusudi, huku rubani mwenzake akiwa amefungiwa nje
ya chumba cha kuongozea ndege.
Bw. Robin amesema rubani Lubitz
alikuwa kimya kabisa wakati rubani mwenzake akihangaika kuingia
kwenye chumba cha kuongozea ndege.
Polisi wakiilinda nyumba ya rubani Lubitz
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni