Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,JoshuaNassar akiwa
ameongozana na baadhi ya wananchi wa jimbo hilo kutembelea eneo hilola Shamba
akiungana mkono na hatua hiyo ya wananchi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Nkoaranga na Poli
wameingia katika Shamba la Karamu (Karamu Estate) usiku wa manane na kuamua
kuotesha migomba kwa kile wanachodai kuchoshwa na serikali kushindwa kusikia
kilio chao cha kurudisha ardhi ya mashamba makubwa yaliyomilikiwa na walowezi
wakati wa ukoloni.
Shamba hilo linalodaiwa kuwa na zaidi ya Hekari 3500
lilivamiwa na wananchi hao na kuanza zoezi la kuotesha migomba kabla ya
kuning'iza mabango yenye ujumbe
mbalimbali katika maeneo tofauti ya shmaba hilo.
Wakizungumza kwa sharti la kutotaja majina yao,wananchi hao
walisema mashamba hayo enzi za ukoloni yalipelekea Wananchi wa Meru kuchangia
fedha kwenye Vyungu na kwamba mwaka 1952 alitumwa marehemu Shujaa Japhet Kirilo
kwenda umoja wa mataifa (UNO)kudai ardhi hiyo.
"Mwaka 1952 tulimtuma Shujaa wetu Kirilo kwenda umoja
wa mataifa (UNO) huko New York nchini Marekani kwenda kudai ardhi hii ya wana Meru lakini
hadi leo hii mwaka 2015 maeneo mengi hayajarudi mikononi mwa
wazawa."alisema mmoja wa wananchi hao.
Akizungumzia hatua hiyo Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki
Joshua Nassari alisema: "Binafsi nikisaidiwa na Mhe. Halima Mdee,Waziri
Kivuli wa Ardhi,tumepiga kelele vya kutosha Bungeni, serikali sikivu bado
haijasikia kelele zetu. Pengine sasa Waziri Lukuvi na serikali hii ya CCM
itasikia kilio cha wananci hawa walioamua kuingia shambani na kuotesha
Migomba"alisema Nassari.
Alisema Shamba la Karamu lilikuwa likitumika kwa kilimo cha
Kahawa na kwamba kwa sasa limegeuka pori huku mwekezaji akidaiwa kuuza kuni kwa
wenyeji na kukodishiwa kulima bustani ndogo ndogo za mboga.
Nassari alidai kuwa hivi karibuni mwekezaji alidaiwa kumega
eneo la shamba hilo na kisha kuliuza kwa chuo kikuu cha Tumaini, tawi la
Makumira na kwa baadhi ya wageni kutokana na kile kinachodaiwa kumalizika kwa
muda wa umiliki wa miaka 99.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni