.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 16 Machi 2015

WASANII WAKUMBUSHWA KUTUMIA FANI YAO KUHAMASISHA AMANI NA UTULIVU NCHINI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wasanii 11 wa Kizazi kipya wanaoendesha Tamasha la Uzalendo Tanzania kabla yha kulizindua rasmi kwenye uwanja wa amani Mjini Zanzibar.
Balozi Seif akitoa hotuba ya kulizindua Tamasha la Uzalendo Tanzania kwenye uwanja wa Amani lililoshuhudia na mamia ya wapenda burden hapa Zanzibar.
Msanii wa Kizazi Kipya Miki wa Pili akitoa shukrani kwa Serikali zote mbili Nchini Tanzania kuunga mkono kazi za wasanii zilizokuwa hazitambuliwi katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Mashabiki wa Burudani ndani ya Viunga vya Mji wa Zanzibar wakiserebuka kwenye Tamasha la Uzalendo Tanzania lililofanyika katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Umati wa mashabiki wa Burdani wakishuhudia waimbaji mbali mbali wa Kizazi Kipya wakifanya vitu vyao katika Jukwaa maalum lililojengwa pembezoni mwa Uwanja wa amani kwenye Tamasha la Uzalendo Tanzania.

                                                                                Picha na – OMPR – ZNZ.
 
Kundi la wasanii kumi na moja wa kizazi kipya Ndani ya Tanzania leo limeuvamia uwanja wa michezo Amani kufanya Tamasha la Pili la Uzalendo Tanzania la Mwaka 2015.

Tamasha hilo lililoasisiwa Mwaka Jana Mjini Dodoma na Rais wa Jamuhuri ya Muungano w Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete lina lengo la kueneza ujumbe wa kudumisha amani na Umoja Miongoni mwa Watanzania wote.

Mamia ya Vijana na wapenda burdani walionekana kumiminika katika uwanja huo wa amani kushuhudia waimbaji maarufu wa Kikazi kipya wakifanya vitu vyao jambo ambalo liliwafanya wengi wa mashuhuda hao kuwacha viti vyao na kuanza kuserebuka.

Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba wasanii Nchini Tanzania wana dhamana kubwa katika kuhakikisha Taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu kupitia fani yao ya sanaa.

Akilizindua Tamasha la Pili la Uzalendo Tanzania la Mwaka 2015 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema wasanii ndio kioo cha jamii kinachoweza kutumika katika kufikisha ujumbe na hata masuala ya maendeleo ya Kijamii.

Alisema mchango wa wasanii katika jukumu kubwa linalolikabili taifa ndani ya mwaka huu wa 2015 kwenye kura ya maoni sambamba na uchaguzi Mkuu wa Mwezi wa Oktoba ni muhimui sana.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba wasanii hao kuhakikisha kwamba suala la Amani linakuwa ndio dira itakayowapa mwanga wa kuendeleza shughuli zao za sanaa popote pale Nchini Tanzania.

Alisema Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ni kisiwa cha amani Duniani. Hivyo juhudi za pamoja kati ya wasanii na wananchi zinahitajika ili kuona lulu hiyo ya amani Nchini Tanzania inaendelea kudumu.

Mapema Mjumbe wa Kamati ya Tamasha hilo Nd. Shaib Ibrahim Mohammed alisema kwamba hilo ni tamasha la kwanza kufanyika hapa Zanzibar likiwa na ujumbe wa kuendelea kusisitiza umuhimu wa kudumisha amani, Umoja na Upendo miongoni mwa Jamii hapa Tanzania.

Akitoa shukrani mwa niaba ya Kundi hilo Msanii Miki wa Pili alizishukuru na kuzipongeza Serikali zote mbili Nchini Tanzania kwa kufahamu umuhimu na mchango wa Wasanii.

Miki alisema fani ya sanaa ndani ya ardhi ya Tanzania ilikuwa ikitambuliwa kama kazi ya kihuni katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Alisema Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wana haki ya kupongezwa kwa kujenga historia ya kudumu iliyoainisha umuhimu wa kutambiliwa kwa kazi za wasanii na kupelekea kuingizwa ndani ya Katiba inayopendekezwa.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni