Abira sita wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya Tumbi iliyopo wilayani Kibaha mkoani Pwani kwa matibabu baada ya basi la Princes Muro walilokuwa wakisafiria kutoka mkoani Arusha kwenda jijini Dar es Salaam kupasuka tairi la mbele na kupinduka katika eneo la Mbwewe, wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Kamanda wa polisi mkoani humo, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na kusema kuwa basi hilo lenye namba za usajili, T 551 BQP lilikuwa na abiria 55 na lilikuwa katika mwendo wa wastani ndio maana halikusababisha maafa makubwa baada ya kupasuka tairi hilo na kupinduka.
Kamanda Matei amesema wanamshikilia dereva wa basi hilo kwa mahojiano zaidi na wamechukua sampuli ya tairi hilo ili kuthibitisha ubora wake.
Pichani ni baadhi ya wasamaria wema na abiria wakijaribu kuwanasua abiria wengine waliokuwa wamenasa ndani ya basi hilo na kutoa mizigo yao.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni