.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 16 Aprili 2015

BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA ATEMBELEA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

unnamed
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkaribisha Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na China katika masuala ya uendelezaji wa Ardhi na Mipango miji.
LUK1
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia) akimweleza Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing (kushoto) namna Wizara yake inavyoendelea kuimarisha shughuli za Mipango Miji ,Usimamizi na Matumizi endelevu ya Ardhi katika maeneo mbalimbali LUK2
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia) akiwa katika mazungumzo na ugeni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania uliomtembelea leo Ofisini kwake ukiongozwa na Balozi Lu Youqing (kushoto) kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya China na Tanzania katika kuimarisha shughuli za Mipango Miji ,Usimamizi wa Matumizi endelevu ya Ardhi .
LUK3 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Alphayo Kidata (kushoto) akifurahia jambo wakati akizungumza na ugeni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania ulioitembelea Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuendeleza ushirikiano kati ya China na Tanzania katika Matumizi endelevu ya Ardhi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni