.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 20 Aprili 2015

DR KAMANI AWAASA WANAFUNZI WA KIKE KUZINGATIA MASOMO YAO NA KUEPUKA VISHAWISHI


                                                                                 Na:Shushu JoeLBusega.

WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi nchini ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Busega, Dr Titus Kamani amewataka wanafunzi wakike walio maliza darasa la saba katika shule za msingi wilayani Busega kuepuka mafataki ambao wamekuwa wakiwalaghai kwa kuwapa zawadi ili waweze kuingia katika mtego wa mapenzi.

Kauli hiyo ameitoa jana wilayani Busega mkoani Simiyu alipokuwa anaweka jiwe la msingi katika shule ya msingi Masanza na kuongea na wazazi wa wanafunzi hao.

Alisema kuwa kuna tabia mbaya inayofanywa na baadhi ya wanaume (mafataki) wanaotumia fedha zao kwa kuwadanganya watoto wakike na kisha kuwaingiza katika mapenzi hali ambayo pia inachangia kuvuruga masomo yao.
 

Alisema kuwa, kila mtoto anapaswa kujilinda na matendo maovu ikiwemo ya madawa ya kulevya na pia waepuke tamaa ya kutaka kupewa vizawadi vidogovidogo kutoka kwa wanaume kwa sababu msingi mkubwa wa maisha yao ni kupata elimu, alisema Dr kamani .


Katika hafla hiyo fupi Kaman aliwaomba wazazi wa eneo hilo kuwa karibu sana na walimu ili waweze kuwapa watoto wetu elimu iliyo bora na waweze kuwa viongozi wetu wa baadaye kwani hata maneno ya mungu yanasema kuwa usimwache elimu aende zake, mara baada ya hafla hiyo fupi waziri kamani aliwaahidi wananchi wa kiloleli kuwa atatoa mabati 100 na mifuko ya cement 100 kwa ajili ya kumalizia darasa liliokuwa alijamalizika shuleni hapo.

Waziri huyo aliongeza kuwa anatambua uwepo wa changamoto katika mambo ya elimu na hivyo aliwasihi wazazi kuwa na mshikamano wa hali ya juu kuliko walivyo sasa ili sekta ya elimu iweze kuwa juu wilayani busega, tusiwe wagumu kuchangia maendeleo yetu na pia aliwataka kuwa na umoja, ingawa aliwaambia maendeleo sio porojo nadhani wenyewe mnaona kamn anafanya nini jimbo kwake .

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw, Msiba Chibuga alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi lakini tunatoa pongezi zetu za dhati kwa mbunge wetu ambaye pia ni waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi kwa msaada wake wa mabati na cement na hivyo kuahidi kuitumia kwa shughuli zilizolengwa.







Hakuna maoni :

Chapisha Maoni