Timu ya soka ya Chelsea imeendelea kujiimarisha kileleni katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kuifunga Manchester United bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu nchini humo uliochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge.
Bao pekee la ushindi la matajiri hao wa jiji la London lilifungwa na Eden Hazard katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
Kwa ushindi huo, Chelsea imefikisha pointi 76 wakifuatiwa na Arsenal walio katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 66 ili hali Manchester United wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 65.
Eden Hazard akikosa kufunga bao la pili
Aliyekuwa kocha mkuu wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ( mwenye miwani ) akiufuatilia mchezo huo uliomalizika kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Aaaah mwamuzi hapanaaa!! Kocha mkuu wa Manchester United, Louis van Gaal akilalamika wakati wa mchezo huo
Vijana vipi goli moja halitoshi!! Kocha mkuu wa Chelsea, Jose Mourinho akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Safiii!! Mmiliki wa Cheslea, Roman Abramovich ( kulia ) akifurahi baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa






Hakuna maoni :
Chapisha Maoni