Goli la dakika ya 88 lililowekwa kimiani na mshambuliaji mviziaji Javier Hernandez lilitosha kuwavusha toka hatua ya robo fainali hadi hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya timu ya soka ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wa marudiano uliochezwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Santiago Bernabeu uliomalizika kwa wenyeji kushinda bao 1-0 mbele ya maelfu ya mashabiki wao waliokuwa wakiwashangailia bila kuchoka.
Mabingwa hao watetezi wa kombe hilo walionyesha soka la kiwango na kufanikiwa kuwatesa tena jirani zao Atletico ambao katika mchezo wa awali uliochezwa Vicente Calderon timu hizo hazikufungana.
Hii ni mara ya pili Real Madrid kuwapa uchungu mashabiki wa Atletico, kwani katika mchezo wa fainali wa ligi hiyo uliozikutanisha timu hizo mjini Lisbon, Ureno mwaka jana, Real Madrid waliwafunga na kutwaa ubingwa wa Ulaya.
Maelfu ya mashabiki wa timu ya Real Madrid wakiipokea timu yao kabla ya mchezo wa marudiano wa klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Atletico Madrid usiku wa kuamkia leo, mchezo uliomalizika kwa Real Madrid kushinda goli 1-0.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)






Hakuna maoni :
Chapisha Maoni