Mshambuliaji mahiri wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akionyesha ufundi wake wa kumiliki mpira huku akiangaliwa na mwenzake, Karim Benzema wakati wa mazoezi ya timu hiyo kabla ya kuvaana na Atletico Madird baadaye usiku leo katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Wachezaji wa Real Madrid wakiwa mazoezini
Kocha mkuu wa Atletico Madrid, Diego Simeone akionyesha umahiri wa kumiliki mpira wakati wa mazoezi ya timu yake.
Ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya robo fainali itaunguruma leo usiku kwa michezo miwili, Real Madrid wakicheza na Atletico Madrid wakati Juventus watakuwa wanavaana na Monaco.
Hata hivyo mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa ni kati ya Real Madrid dhidi ya jirani zao Atletico Madrid.
Mchezo huu utarudisha kumbukumbu ya fainali ya mwaka jana katika jiji la Lisbon, Ureno ambapo timu hizi zilikutana na Real Madrid wakatwa ubingwa kwa kuwachapa Atletico Madrid mabao 4-1 na kunyakua kombe hilo kwa mara ya 10.
Mchezo wa leo, Atletico watakuwa nyumbani katika uwanja wao wa Vicente Calderon ambao upo katika kitongoji cha Arganzuela katika jiji la Madrid.
Wachezaji wa Atletico Madrid wakisikiliza maelekezo ya kocha wao wakati wa mazoezi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)








Hakuna maoni :
Chapisha Maoni