Timu ya soka ya Chelsea imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Uingereza baada ya jana kulazimishwa sare ya kutofungana na Arsenal katika mchezo wa ligi kuu nchini humo uliochezwa uwanja wa Emirates.
Katika mchezo huo, timu zote zilionyesha soka la kushambulia, lakini hakuna timu iliyofanikiwa kutikisa nyavu za mwenzake. Kwa matokeo hayo, Cheslea imefikisha pointi 77 wakati Arsenal wakiwa nafasi ya tatu na pointi 67.





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni