Kivumbi cha ligi kuu nchini Uingereza kitaendelea hii leo katika viwanja mbalimbali, lakini mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka ni mchezo kati ya washika bunduki wa jiji la London, Arsenal ambao watakaokuwa nyumbani katika uwanja wao wa Emirates kucheza na Liverpool.
Arsenal wana pointi 60 wakiwa katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo huku Liverpool wakiwa katika nafasi ya tano wakiwa na pointi 54.
Liverpool wanashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-1 na Manchester United mchezo uliochezwa March 22’ 2015 Anfield, wakati Arsenal wao waliwatandika Newcastle 2-1 mchezo uliochezwa March 21’2015.
Mchezo mwingine ni kati ya vinara wa ligi hiyo Chelsea ambao watakuwa nyumbani darajani kucheza na Stoke City.
Mechi nyingine hii leo ni kama ifuatavyo:-
Everton vs Southampton
Leicester vs West Ham
Manchester United vs Aston Villa
Swansea vs Hull
West Brom vs QPR

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni