Mshambuliaji wa Hull City Michael Dawson akiwa ameruka juu na kuupiga kichwa mpira uliomshinda mlinda mlango wa Liverpool, Simon Mignolet na kujaa moja kwa moja wavuni.
Timu ya soka ya Liverpool imeendelea kujiweka pabaya kushindwa kuingia nne bora, baada ya jana usiku kukubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa Hull City katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza.
Katika mchezo huo, bao la wenyeji lilifungwa na Michael Dawson kwa kichwa kunako dakika ya 37 ya kipindi cha kwanza.
Kwa matokeo hayo Liverpool wamesimama katika nafasi ya tano wakiwa na jumla ya pointi 58 huku Hull wakiwa katika nafasi ya 15 wakiwa na pointi 34.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni