.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 23 Aprili 2015

LIGI YA MABINGWA ULAYA JUVENTUS YASONGA MBELE HATUA YA NUSU FAINALI, MONACO SAFARI YAISHIA NYUMBANI KWAO

Wachezaji wa timu ya soka ya Juventus ( bibi kizee cha Turini ) ya Italia wakishangilia kufuzu kwa hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Timu ya soka ya Juventus ya Italia imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya usiku wa kuamkia leo kufanikiwa kutoka sare ya kutofungana na wenyeji wao Monaco ya Ufaransa. 

Huu ulikuwa mchezo wa marudiano wa robo fainali ya ligi hiyo, baada ya mchezo wa awali uliochezwa nchini Italia wiki iliyopita, Juve kuifunga Monaco bao 1-0. 

Juventus imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali kwa faida ya ushindi wa mchezo wa awali.

Juventus imefanikiwa kuingia hatua hii ya nusu fainali toka mwaka 2003.






Hakuna maoni :

Chapisha Maoni