.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 16 Aprili 2015

MAFUNZO YA MAFUTA NA GESI ASILIA CHINA - SMZ

01
Maafisa Waandamizi wa SMZ wakiwa katika viwanja vya Tiananmen Square Jijini Beijing China, wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Mhandisi Mwalim Ali Mwalim na aliyevaa tai ni Mhandisi wa Idara ya Nishati, Omar Saleh Mohamed na wengine mwenye traksuti ni Afisa Mdhamini WQizara ya Ardhi, Makaazi Maji na Nishati Pemba, Mhandisi wa Miamba, Hemed Salim.
02 
Maafisa Waandamizi wa SMZ wakiwa viwanja vya Tiananmen Square wa mbele kabisa ni Mkurugenzi wa Usalama kazini, Mhandisi Suleiman Khamis kushoto ni Mwandishi wa habari Juma Mohammed na kulia ni Mhandisi wa Idara ya Nishati, Omar Saleh Mohamed.
04
Wakurugenzi wa SMZ wakiteta jambo walipotembelea viwanja vya Tiananmen Square Jijini Beijing China. Wakurugenzi hao ni miongoni mwa Maafisa 20 waandamizi wa SMZ wanaohudhuria mafunzo ya muda mfupi ya mafuta na gesi asilia. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Mipango Sera na Utafiti, Salhina Ameir Mwita, anafuatia mwenye kamera ni Mkurugenzi wa Idara ya Nishati, Mohamed Abdalla Mohamed, mwengine ni Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi,Makaazi Maji na Nishati Pemba, Hemed Salim na mwisho ni Mkurugenzi wa Usalama Kazini, Suleiman khamis.
03
Maafisa Waandamizi wa SMZ wakiwa katika viwanja vya Tiananmen Square Jijini Beijing China. Maafisa hao wanahudhuria mafunzo ya muda mfupi ya mafuta na gesi asilia.  

                                                                                      (Picha na Al-Amin Omar)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni