.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 20 Aprili 2015

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR, MAALIM SEIF AKUTANA NA BALOZI MDOGO WA INDIA


(Picha na Salmin Said, OMKR)

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amekutana na balozi mdogo wa India aliyepo Zanzibar balozi Satendar Kumar, na kueleza kuwa Zanzibar inayo mambo mengi ya kujifunza kutokana na uzoefu wa India.
Ametaja mambo hayo kuwa ni pamoja na mawasiliano ya habari (ICT) pamoja na maeneleo ya sekta ya afya.
 
Amesema India imepiga hatua kubwa katika maeneo hayo, na kwamba itashirikiana na nchi hiyo katika kuhakikisha kuwa vijana wa Zanzibar wanapata utaalamu wa kutosha na kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi.
 
Ameishauri India ambayo imekuwa miongoni mwa nchi tatu zinazowekeza zaidi nchini, kuendelea kuweka vitega uchumi vyao ambavyo vinasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Aidha ameishauri nchi hiyo kuangalia uwezekano wa kushirikiana na Zanzibar katika kuvifufua viwanda vilivyopo nchini, ili viweze kufanya kazi.
Naye balozi Satendar Kumar amemuhakikishia Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa India itaendelea kushirikiana na Zanzibar katika maeneo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kukuza biashara pamoja na kuendeleza miradi iliyoanzishwa na nchi hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni