.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 21 Aprili 2015

MISAADA ZAIDI YAENDELEA KUPOKELEWA KIJIJI CHA LAMADI WILAYANI BUSEGA

Mkuu wa wilya ya Busega, Mh Paul Mzindakaya ( kushoto ) akipokea msaada kwa ajili ya waathirika wa mafuriko katika kijiji cha Lamadi kutoka kwa mmoja wa mwananchi.

                                                                              Na Shushu joel,Busega

MKUU wa wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya amewapongeza wale wote waliojitolea kuwasaidia waliopatwa na mafuiko mwanzoni mwa mwezi huu katika kijiji cha lamadi wilayani Busega, mkoa wa Simiyu.

Akitoa pongezi hizo ofisini kwake, Mzindakaya alisema kuwa cha kuwalipa akioni bali Mungu aliye na mapenzi makubwa kwetu anajua ni kiasi gani watu hao wema wao umetumika katika wilaya yake ya Busega.

Aliongeza mpaka sasa amepata misaada mbalimbali kutoka kwa watu na taasisi ambazo kwa ukweli zimetumika kwa waathika wa mafuriko hayo ambayo yamekosesha watu 1686 makazi.

Mzindakaya aliwapongeza wale wote waliojitolea kwa hali na mali ili kuhakikisha watanzania wenzao wanapata japo mahitaji muhimu ya kibinadamu ikiwemo chakula,mavazi na madawa.

Aliongeza kuwa anamwagia sifa za pekee mbunge wa jimbo la la Busega na Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi nchini Dk Titus Kaman kwa wema wake wote aliouonyesha kwa waathirika hao wa kijiji cha lamadi, kwani alitoa misaada mingi nay a kutosha kwa wale wote waliopatwa na matatizo hayo.

Pia amewapongeza wananchi wote wa lamadi kwa kuonyesha umoja,upendo na mshikamano wao kwa kuweza kuwahifadhi wale wote waliopatwa na mafuriko na hata kuweza kuwapa mavazi na kuwataka watu hao waweze kuendelea na moyo huo.

Aidha Mzindakaya amewataka waathirika hao kuwa na utulivu wa hali juu kwa kipindi hiki kwani serikali inalishughulikia suala lao kwa ukaribu wa hali ya juu ili kuhakikisha waathirika wote wanapata mahitaji yao ya msingi.

Mpaka sasa watendaji wote toka halmashauri ya wilaya ya Busega kwa kushirikiana na kamati ya maafa ya kata ya lamadi wanamalizia kufanya tasimini ya uhakika ili kuweza kubaini ni mahitaji gani yanahitaji kwa watu hao wote waliopatwa na mafuriko hayo ndani ya kijiji cha lamadi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni