.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 28 Aprili 2015

MKUTANO WA MAWAZIRI WA SADC WAANZA NCHINI ZIMBABWE

Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe, Mhe. Simbarashe Mumbengegwi akifungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaojadili Mkakati na Mwongozo wa kuelekea Maendeleo ya Viwanda katika Kanda ya SADC. Mhe. Mumbengegwi amefungua mkutano huo jijini Harare, Zimbabwe huku akiwa na huzuni kubwa kufuatia taarifa ya kifo cha Bregedia Jenereli Hashim Mbita ambaye alitoa mchango mkubwa katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika. Mhe. Mumbengegwi aliwaomba wajumbe wote wa mkutano kusimama ili kumuombea dua Bregedia Hashim Mbita.Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (Mb) wa katikati akiomba dua kumkumbuka Brigedia Hashim Mbita. Kulia kwa Mhe, Kigoda ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) nao pia wakimuombea dua Brigedia Mbita.  Meza kuu nayo ikimtakia kheri Brigedia Hashim Mbita.Katibu Mtendaji wa SADC, Bi. Stergomena Tax akitoa hotuba kwa Baraza la Mawaziri wa SADC.Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe, Mhe. Simbarashe Mumbengegwi akitoa hotuba ya ufunguzi ya Mkutano wa Baraza la Mawziri wa SADC.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe akiangalia hotuba aliyekabidhiwa na Katibu Mtendaji wa SADC, Bi. Tax mara baada ya kuwasilishwa na Katibu Mtendaji huyo mbele ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADCKutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb); Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (Mb); Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) wakiwa na Mawaziri wa nchi nyingine katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC.Makatibu Wakuu wakiwa katika kikao cha maandalizi. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni