.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 3 Aprili 2015

MPAKA KUFIKIA SASA WANAFUNZI 147 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KIKUNDI CHA AL SHAABAB KUFANYA SHAMBULIZI KATIKA CHUO KIKUU CHA GARISSA NCHINI KENYA JANA

Mpaka kufikia sasa imethibitishwa kuwa,  jumla ya wanafunzi 147 wameuawa na wengine 79 wamejeruhiwa baada ya kundi la kigaidi la Al Shaabab kufanya shambulio katika Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya mapema jana asubuhi. 

Tukio hilo limetokea jana saa kumi na moja alfajiri. Katika operesheni kabambe iliyoendeshwa na jeshi katika kupambana na magaidi hao, jumla ya wanafunzi 587 walifanikiwa kuokolewa salama.
             Mmoja wa wanafunzi aliyejeruhiwa katika tukio hilo akipatiwa msaada
Askari wa jeshi la Kenya akiwa amekizingira chuo hicho huku wengine wakimsaidia mmoja wa wanafunzi hao.
Askari wa jeshi la Kenya wakiwasili katika chuo hicho tayari kukabiliana na magaidi hao.
Mmoja wa wanafunzi akiondolewa katika maeneo ya chuo hicho baada ya kutokea shambulizi lililoua wanafunzi wenzake 147 na kujeruhi wengine 79.
                                             Tuko imara, tutapambana nao mpaka tuwamalize.






Hakuna maoni :

Chapisha Maoni