Robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ukiwa ni mchezo wa marudiano utaunguruma leo katika viwanja viwili, lakini mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa ni kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid.
Mchezo huo utakaochezwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa, kwani Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo watakuwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha hawavuliwi taji kwa kukubali kufungwa na Atletico hivyo kushindwa kufuzu kwa hatua ya nusu fainali ya ligi hiyo.
Katika mchezo wa awali uliochezwa Vicente Calderon, timu hizo hazikufungana.
Mchezo mwingine leo ni kati ya Juventus watakao kuwa ugenini kucheza na Monaco katika uwanja wa Stade Louis II nchini Ufaransa. Katika mchezo wa awali, Juventus waliichapa Monaco 1-0.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni