.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 24 Aprili 2015

NI KIVUMBI NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA, BARCELONA USO KWA USO NA BAYERN MUNICH

Hatimaye Shirikisho la soka barani Ulaya ( UEFA ) limechezesha droo ya hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani humo, ambapo miamba ya soka duniani Bayern Munich itakutana uso kwa uso na FC Barcelona katika hatua hiyo, mchezo wa kwanza ukichezwa Nou Camp kati ya May 5 au 6' 2015. 

Nao mabingwa watetezi wa kombe hilo, Real Madrid watacheza na Juventus ya Italia katika hatua hiyo. Hata hivyo mchezo utakaosubiriwa kwa hamu kubwa ni kati ya Bayern na Barcelona. 

Bayern Munich imeingia hatua hiyo baada ya kuitandika jumla ya mabao 6-1 katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya ligi hiyo timu ya FC Porto ya Ureno hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa mabao 7-4, kwani katika mchezo wa awali mjini Lisbon Ureno, Bayern walifungwa 3-1. 

Wao Real Madrid walifuzu baada ya kuifunga Atletico Madrid bao 1-0. Katika mchezo wa awali timu hizo hazikufungana.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni