.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 28 Aprili 2015

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA MUUNGANO ZAFANYIKA MJINI BEIJING, CHINA

Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Abdulrahman Shimbo (wa tatu kushoto) na mkewe Mama Shimbo (wan ne kushoto), wakiwa na viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Beijing (TZ-SUB) katika sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilizofanyika Ubalozini mjini hapa. Mh Balozi Shimbo alikuwa mgeni rasmi. (Picha na Fabian James)
Balozi wa Tanzania nchini China, Mh Abdulrahman Shimbo akitoa mawaidha kwa waalikwa katika sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilziofanyika Ubalozini mjini hapa. Mh Balozi Shimbo alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Beijing (TZ-SUB).(Picha na Salum Ramadhan)
Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Abdulrahman Shimbo (wa pili kushoto) na mkewe (wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya za Wanafunzi Beijing kutoka nchi za Afrika Mashariki waliohudhuria sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilizofanyika Ubalozini mjini hapa. Balozi Shimbo alikuwa mgeni rasmi. (Picha na Salum Ramadhan )
Wanafunzi Wakitanzania Beijing pamoja na wageni mbalimbali katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Balozi wa Tanzania nchini China, Abdurahman Shimbo (mwenye suti katikati) na mkewe, katika sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilizoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Beijing (TZ-SUB) na kufanyika Ubalozini mjini hapa. (Picha na Fabian James)
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi Beijing (TZ-SUB), Ireneus Kagashe (kulia) akitoa utangulizi katika sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilizofanyika Ubalozini mjini hapa. Wa kwanza kushoto ni mgeni rasmi wa sherehe hizo, Balozi wa Tanzania, China, Mh. Abdulrahman Shimbo, Mkewe Mama Shimbo na Katibu wa Shirikisho la Jumuiya za Wanafunzi nchini China, Michael. (Picha na Salum Ramadhan)
Familia na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China katika picha ya pamoja wakati wa sherehe za miaka 51 ya Muungano zilizofanyika Ubalozini mjini hapa. Sherehe hizo ziliandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Beijing (TZ-SUB). Wa sita kutoka kushoto ni mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Abdulrahman Shimbo, kushoto kwake ni mkewe, Mama Shimbo (Picha na Salum Ramadhan)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni