.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 27 Aprili 2015

UTOAJI NISHANI ZA KUMBUKUMBU YA MIAKA 50 YA MUUNGANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Tanzania wakisimama wakati wimbo wa taifa ukipigwa baada ya kumalizika hafla ya sherehe ya utoaji wa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili,Tatu na Nne jana katika viwanja vya Ikulu Jijini Dares Salaam
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) na makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika sherehe za utoaji wa nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano wa madaraja mbali mbali katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam
Miongoni mwa Viongozi na Wananchi walioteuliwa kutunikiwa nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano wa madaraja mbali mbali wakiwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya kutunikiwa nishani zao ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar jana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha Jaji Mkuu Msataafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha Bw.Mabrouk Jabu Makame Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Bw.Damian Zefrini Lubuva baada ya kumvalisha Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam katika kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha nishani Bw.Aboud Talib Aboud wakati wa hafla ya kutunuku Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akivalisha Nishani Bw,Mohammed Seif Khatibu wakati wa hafla ya kutunuku Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha Cpl Laura Philip Mushi Nishani ya Ushupavu wakati wa utoaji wa Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Madaraja mbali mbali katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Rais wa jamhuri ya Muungano Dk.Mohammed gharib Bilali pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika hafla ya sherehe ya utoaji wa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili,Tatu na Nne jana katika viwanja vya Ikulu Jijini Dares Salaam,[Picha na Ikulu.]

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni