Wapiganaji wa kundi la Al Shaabab wanadaiwa kumteka na baadaye kumuua Chief wa Mandera muda mfupi baada ya kumteka akiwa na abiria wengine wakisafiri kwa basi kutoka Elwak kuelekea Mandera mjini jana saa moja asubuhi.
Wapiganaji hao wanadaiwa kuwa na silaha za moto wakati walipolisimamisha basi hilo, kisha kuwaamuru abiria wote kuteremka chini, kisha wakaanza kukagua nyaraka zao na baadaye kuwapora simu za mkononi, fedha na vitu vingine.
Bada ya tukio hilo, waliwaamuru abiria wengine kuendelea na safari yao huku wakiondoka na Chief huyo kuelekea nae Somalia ambapo baadaye walimuua.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni