AFISA mipango wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Safia Saleh Sultan akijubu hoja za washiriki wa kongamano, lililofuatiwa na hafla ya kuwatunuku vyeti , kongamano hilo lilifanyika mjini Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKURUGENZI mtendaji wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZSLC, Harusi Miraji Mpatani, akielezea dhana ya wasaidizi wa sheria ilivyozaa matunda, ambayo ilianzishwa na kituo hicho tokea mwaka 2007, kwenye mahafali yao ya tatu yaliofanyika ZSSF mjini Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WASANII wa ngoma ya kibati ‘MKOTA NGOMA’kutoka wilaya ya Mkoani, wakitikisha jukwaa kwa kupamba mahafali ya tatu ya wasaidizi wa sheria wa majimbo ya yote ya Zanzibar, yaliofanyika Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WAANDISHI wa habari wa vyombo mbali mbali, wakiwa kazini kwenye mahafali ya tatu ya wasaidizi wa sheria wa majimbo 52 ya uchaguzi, wasaidizi hao wamesomeshwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC kwa muda wa miaka miwili, (Picha na Haji Nassor, Pemba). Kwa hisani ya ZanziNews
BAADHI ya watendaji wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC, wakifuatilia hutuba iliotolewa na rais wa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na haki za watu, jaji Agostino Ramadhan alioitoa kwenye mahafali ya tatu ya wasaidizi wa sheria wa majimbo ya Ugunja na Pemba, yaliofanyika ZSSF mjini Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WASANII wa ngoma ya kibati ‘MKOTA NGOMA’kutoka wilaya ya Mkoani, wakitikisha jukwaa kwa kupamba mahafali ya tatu ya wasaidizi wa sheria wa majimbo ya yote ya Zanzibar, yaliofanyika Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni