.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 21 Aprili 2015

ZAIDI YA WAZIMBABWE 400 WAKIMBIA VURUGU AFRIKA KUSINI

Mamia ya raia wa Zimbabwe waliokuwa wakiishi na kufanya kazi nchini Afrika Kusini wamerejea kwao baada ya kukimbia mapigano nchini humo yanyofanywa na raia wa Afrika Kusini kwa madai kuwa wageni wamechukua ajira zao. 

Katika vurugu hizo baadhi ya wageni wamepoteza maisha, wengi kujeruhiwa huku pia uporwaji ukifanywa na wenyeji hao katika maduka ya raia wa kigeni. 

Zaidi ya Wazimbabwe 400 wamesafiri kwa mabasi kutoka Dublin, Afrika Kusini kurejea kwao wakikimbia ubaguzi huo unaofanywa na wenyeji. 

Zaidi ya raia 3,200 wa Malawi nao wamehifadhiwa katika kambi za muda kusalimisha maisha yao kufuatia vurugu hizo.
Raia wa kigeni ( kushoto ) akishambuliwa na vijana wa Afrika Kusini katika moja ya vurugu zinazoendelea nchini humo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni