Baada ya kumalizika kwa michuano ya
ligi ya mkoa wa Dar es salaam na kupata timu tatu zitakazouwakilisha
mkoa katika michuano ya ligi ya mabingwa ya mikoa ya TFF,kesho
Alhamis Aprili 09/2015,katika uwanja wa Karume jijini kutakuwa na
mchezo wa fainali ya kumpata Bingwa wa jumla wa michuano ya ligi ya
mkoa.
Timu zitakazoumana katika fainali
hiyo ni ZAKHEM FC dhidi ya FFU SC,ambazo zitashuka dimbani majira ya
saa kumi jioni zikishuhudiwa na umati wa mashabiki waliokuwa
wakiyafuatilia mashindano hayo tangu yalipoanza kutimua vumbi.
Kwa mujibu wa kamati ya mashindano
ya chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,timu zilizofanikiwa
kuuwakilisha mkoa katika michuano ya ligi ya maabingwa ni pamoja na
ZAKHEM FC,FFU SC na CHANGANYIKENI SC.
Mwenyekiti wa DRFA,Almas
Kasongo,ameipongeza kamati hiyo ya mashindano kwa kusimamia vizuri
uendeshaji wa ligi tangu ilipoanza.
Imetolewa na DRFA,
Mkuu wa kitengo cha Habari na
Mawasiliano DRFA
Omary
Katanga/+255766358585/+255784500028.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni