Mabondia Adam Ngange wa Chanika Dar es salaam kushoto na Iddi Pialali wa Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa chuo cha sanaa Bagamoyo TASUBA Ngange alishinda kwa point mpambano huo wa raundi sita picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Adam Ngange kushoto wa Chanika akimrushia konde la kulia bondia Iddi Pialala wa Bagamoyo wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa chuo cha sanaa Bagamoyo TASUBA Ngange alishinda kwa point mpambano huo wa raundi sita picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Iddi Pialali wa Bagamoyo akimtupia makonde mfululizo bondia Adam Ngange wa Chanika wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa chuo cha sanaa Bagamoyo TASUBA Ngange alishinda kwa point mpambano uho wa raundi sita picha na SUPER D BOXING NEWSNa Mwandishi Wetu
BONDIA Adam Ngange wa Chanika Dar es salaam amemsambaratisha Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo kwa point katika mpambano wao mkali wa raundi sita uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha sanaa Bagamoyo TASUBA ambapo kulikuwa na shamra shamra za kutosha kwa upande wa Pialali.
Ukumbi ulifurika watu mbalimbali na mashabiki wa kutosha kabisa
Mpambano ulivyoanza ngumi zilianza kupigwa kwa Pialali kwa kumshambulia sana Ngange mnamo raundi za mwanzo lakini kadri mpambano ulivyokuwa unasonga mbele na raundi kuzidi kwenda mbele ndipo Ngange akazinduka na kuanza nae kumshambulia kwa kasi zaidi ambapo mpaka kufika raundi ya sita raundi ambayo ilitawaliwa na Ngange kupiga ngumi za misili ya paka anavyopiga kibao na kurudisha mkono alipo utoa mpaka raundi ya mwisho ya mchezo Ngange alikuwa mshindi kwa point mbili zaidi ya Pialali akika lilikuwa pambano zuri ambalo lilikusanya mashabiki wengi wa mkoa wa Pwani na Dar es salaam
mpambano huo ulileta raha zaidi baada ya kuhudhuriwa na mabondia mbalimbali nchini wakiongozwa na Japhert Kaseba,Thomas Mashali. Said Mbelwa. Shabani Kaoneka na Ibrahimu Tamba mabondia ambao wanatamba kwa sasa nchini Tanzania
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni