.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 7 Mei 2015

BONDIA FLOYD MAYWEATHER AIBUKA KATIKA SHEREHE YA MWANAMUZIKI CHRIS BROWN, AONYESHA JEURI YA FEDHA

Mwanamuziki Chris Brown akiwa ameshika chupa ya Shampeni huku pembeni wasichana  warembo wakiwa wamebeba keki wakati wa sherehe yake ya kutimiza miaka 26 ya kuzaliwa kwake iliyofanyika katika kalbu ya Drai's mjini Las Vegas nchini Marekani. 

Kati ya mastaa waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na bondia Floyd Mayweather ambaye alionyesha jeuri ya pesa. 

Mayweather ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alimpiga mpinzani wake Manny Pacquiao katika ukumbi wa MGM Grande Arena, alionekana akitoa fedha " dola " katika begi maalum lililokuwa limebebwa na mmoja wa wapambe wake alioongozana nao katika sherehe hiyo.
                         Floyd Mayweather akitoa hela katika begi tayari kwa matumizi.
Mnakiona kibunda cha dola mia mia!! Mayweather akiwa ameshika kibunda cha dola mia mia tayari kulipa bili yake wakati wa sherehe ya miaka 26 ya mwanamuziki Chris Brown.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni