.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 18 Mei 2015

FC BARCELONA MABINGWA WA LA LIGA 2014/2015, WAWACHAPA WAGUMU ATLETICO MADRID 1-0

Wachezaji wa FC Barcelona wakifurahia kutwaa ubingwa wa La Liga 2014/2015 mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu nchini Hispania dhidi ya Atletico Madrid, mchezo uliomalizika kwa Barcelona kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Timu ya soka ya FC Barcelona wamefanikwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Hispania hapo jana baada ya kuitungua Atletico Madrid kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Vicente Calderon. 

Bao pekee la Barcelona lilifungwa na mshambuliaji Lionel Messi katika dakika ya 65 ya mchezo huo. 

Barcelona wametwaa ubingwa wakiwa na pointi 93 wakifuatiwa na Real Madrid wenye pointi 89 ili hali Atletico de Madrid wakiwa na pointi 77.



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni