Idadi ya vifo kutokana na joto
nchini India imefikia watu 800, huku kiwango cha joto katika taifa
hilo kikifikia nyuzi joto 50 katika baadhi ya maeneo.
Vifo vingi vimetokea katika majimbo
la kusini la Telangana pamoja na Andhra Pradesh, ambako zaidi ya watu
750 wamekufa tangu wiki iliyopita.
Watu wengine 24 wamekufa kutokana na
joto kali katika maeneo ya West Bengal pamoja na Orissa.
Hospitali zimetakiwa kuwa katika
tahadhari ya kutibu wagonjwa wa moyo na mamlaka zimewataka watu kukaa
nyumbani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni