.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 21 Mei 2015

LIGI KUU ENGLAND, SUNDERLAND YANUSURIKA KUTEREMKA DARAJA NI BAADA YA KULAZIMISHA SARE NA ARSENAL USIKU WA KUAMKIA LEO

Timu ya soka ya Sunderland imenusurika kuteremka daraja msimu ujao, baada ya usiku wa kuamkia leo kulazimisha sare ya kutofungana na washika bunduki wa jiji la London, Arsenal katika mchezo wa ligi kuu nchini England uliochezwa katika uwanja wa Emirates.
Kwa matokeo hayo ya kutoka uwanjani timu hizo zikiwa hazijafungana, Sunderland imefikisha pointi 38 ikiwa nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi hiyo, na sasa timu ambazo mwakani hazitakuwa katika ligi kuu England, yaani zinateremka daraja ni Qeens Park Rangers ( QPR ) iliyomkiani ikiwa na pointi 30 pamoja na Burnley iliyo na pointi 30.
Baada ya kukamilika kwa mchezo huo, wachezaji, kocha pamoja na mashabiki wa Sunderland walilipuka kwa furaha baada ya kujihakikishia kubaki ligi kuu England.




Hakuna maoni :

Chapisha Maoni