Mabingwa wa ligi kuu nchini England, Chelsea wamejikuta wanaharibu sherehe zao za ubingwa wa msimu huu wa 2014/2015 wa ligi hiyo baada ya usiku wa kuamkia leo kukubali kipigo kikali cha mabao 3-0 toka kwa West Brom ambao wapo katika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi hiyo.
Wakicheza ugenini, Chelsea walishuhudia wakifungwa mabao hayo yaliyowekwa kimiani na wachezaji Saido Berahino aliyefunga mabao mawili katika dakika za 9 na 47 na Chris Brunt akifunga bao la tatu katika dakika ya 60.
Mlinda mlango wa Cheslea, Courtois akiruka bila mafanikio kuuzia mpira uliojaa wavuni.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni