Timu ya soka ya Liverpool imeshindwa kukata tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kushindwa kuingia nne bora katika ligi kuu ya Uingereza inayoelekea ukingoni.
Wakicheza katika uwanja wa ugenini, Liverpool walijikuta wakilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na mabingwa wa ligi hiyo Chelsea. Wenyeji ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa nahodha wake, John Terry kwa kichwa kabla ya Liverpool kusawazisha pia kupitia kwa nahodha wake Steven Gerald kwa kichwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni