Mabalozi hao wa Usalama Barabarani nchini walipata fursa ya kuhudhuria kikao cha Bunge mjini Dodoma hapo jana wakati wa kuwasilishwa kwa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchini, na baadaye kufanya kikao cha ndani na Naibu Waziri huyo kujadili hali ya usalama barabarani.
Toka uwepo wa mabalozi hawa kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani, kwa kiasi kikubwa wamekuwa msaada mkubwa wa kupungua kwa ajali za barabarani zinazosababishwa na uzembe wa baadhi ya madereva.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni