.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 6 Mei 2015

MAHAKAMA YAMTIA HATIANI MUIGIZAJI NYOTA WA BOLLYWOOD SALMAN KHAN

Mahakama nchini India imemtia hatiani muigizaji nyota wa Bollywood, Salman Khan kwa kumuua mtu asiye na makazi katika tukio la mwaka 2002 la kugonga watu kwa gari na kisha kukimbia Mjini Mumbai.

Mtu huyo mwanaume aliyekufa ni miongoni mwa watu watano waliogongwa kwa gari, ambapo muigizaji huyo alifunguliwa mashtaka ya mauaji.

Katika utetezi wake Khan amesema dereva wake alikuwa ndie anaendesha gari, lakini Jaji amesema muigizaji huyo ndiye aliyekuwa anaendesha gari huku akiwa amelewa. Hukumu bado haijatajwa na anakabiliwa na kifungo kisichozidi miaka 10.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni