Shirika la Save the Children
limesema makumi ya wahamiaji haramu wamekufa maji katika bahari ya
Mediterranean baada ya boti inayokadiriwa kubeba watu 137 kuzama
kusini mwa Sicily.
Shirika hilo limesema manusura
wameeleza kuwa wengi wa watu walitumbukia baharini wakati mashua ya
uokoaji ikikaribia.
Watu wapatao 1,750 wamekufa katika
mwaka huu wakijaribu kukatiza Mediterranean, ikiwa ni ongezeko mara
20 ikilinganishwa na mwaka jana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni