Mamia ya wananchi wa jimbo la Mvomero mkoani Morogoro wakimpokea kwa shangwe Mbunge wao Mh Amos Makalla
Mh Amos Makalla ( mwenye miwani ) akiongozana na wananchi wa jimbo lake la Mvomero wakati wa mapokezi yake jimboni humo.
Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa jimbo la Mvomero mkoani Morogoro, Mh Amos Makalla akiwahutubia wananchi wa jimbo lake la Mvomero.
Mbunge wa jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla ameendelea na ziara ya kikazi jimboni kwake huku makundi mbalimbali yakiendelea kumuunga Mkono na kumshawishi achukue fomu ya ubunge kwa kipindi kijacho.
Katika ziara yake ya kichama, amekagua kazi zinazofanywa na kikundi cha akina mama wanaofinyanga vyungu, akinamama wajasiriamali wauza kokoto na walima bustani.
Aidha amezindua Shina la ushindi ambalo wakina mama wafinyanga vyungu ndiyo wanachama wa Shina hilo.
Katika kuunga mkono vikundi hivyo, mbunge huyo amewachangia pump ya kumwagilia na fedha vyote kwa pamoja sh 2,800,000.
Wakitoa ujumbe kupitia nyimbo, akina mama hao wamemtaka mbunge wao muda ukifika achukue fomu kwani wameridhishwa na kazi Nzuri alizozifanya kijijini hapo ukiwepo umeme na huduma za jamii.
Akihutubia katika mkutano huo,Mh Makalla aliwapongeza kwa kujiunga katika vikundi na mafanikio yanaonekana.
Amewapongeza kwa bidhaa nzuri za majiko, vyungu na upatikanaji wa kokoto kwa urahisi na kwa bei nafuu. Amewahakikishia ushirikiano wa dhati na atachukua fomu kutetea nafasi yake mara muda utakapofika.
Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa mmoja wa wananchi wa jimbo lake.
Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla akikabidhi fedha taslimu kwa ajili ya ununuzi wa pump ya maji kwa vikundi katika jimbo lake.
Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla akifurahia jambo na baadhi ya wananchi wa jimbo lake baada ya kumaliza kuongea nao.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni