Wananchi wa jimbo la Mvomero mkoani Morogoro wakimpongeza mbunge wao na Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla.
Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla akiwahutubia mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza
Mnunge wa Mvomero, Mh Amos Mkalla akihutubia mkutano kijiji cha Kichangani kuhusiana na hatua za dharura kurejesha huduma Maji vijiji vya Kichangani,Mhonda, Manyinga na Madizin.
Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akipelekwa kwenda kuona tanki la maji katika kijiji cha Kichangani litakaloingizwa maji katika hatua za dharura.
Wananchi wa jimbo la Mvomero waliohudhuria mkutano uliohutubiwa na mbunge wao, Mh Amos Makalla wakimpongeza mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Serikali imechukua hatua za dharura kuwapatia maji wananchi wa Vijiji vya Kichangani, Mhonda , Manyinga na Madizini baada ya kuchelewa kwa mradi wa maji Turiani kutokana na kasoro za kisheria zilizopelekea mkandarasi kusimama kujenga mradi huo akidai nyongeza za malipo.
Uamuzi wa kuchukua hatua za dharura ulitangazwa jana na mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kichangani ambapo aliwaeleza wananchi wa Vijiji hivyo sababu za kuchelewa kwa mradi huo, na kutokanana na tatizo kubwa la maji wizara yake wakati mradi unaendelea kutekelezwa utaingiza maji katika matanki ya zamani ya kichangani na mhonda na kuweka matanki mengine ya simtank kwa ajili ya kijiji cha madizini na manyinga na kuyaingiza katika mtandao mpya wa mabomba ili wananchi waanze kupata maji.
Aidha ameipa masaa 24 serikali ya kijiji cha kichangani kuacha mara moja kuwachangisha wananchi fedha kwa ajili ya kugharamia urejeshaji wa huduma ya Maji, na ameuagiza uongozi huo kuwarejeshea wananchi Fedha zote walizokuwa wamechangishwa kwa kisingizio cha kurejesha huduma ya Maji.
Akionekana kukerwa na ubabaishaji unaofanywa na viongozi wa serikali ya kichangani inayoongozwa na Chadema na undumila kuwili wa kauli zao alisema" Nyie tarehe 12 desemba mwaka jana wakati wa uchaguzi wa vitongoji na vijiji mlisema mkichaguliwa tu mtapiga marufuku michango yote na mkichaguliwa tu tarehe 14 desemba Siku inayofuata maji yatatoka hapa.
Mbona leo ni miezi 5 maji hayajatoka? Na inakuaje mnachangisha wananchi na mlisema maendeleo yatapatikana bila kushirikisha michango ya wananchi?
Kwakuwa yote haya yameshindikana na kwakuwa si sera yenu kushirikisha wananchi naagiza na ninawapa masaa 24 mrejeshe fedha zote mlizowachangisha wananchi na serikali itarejesha huduma ya Maji kupitia fungu la dharura lililopo katika mkataba baina ya serikali na mkandarasi
Baada ya kauli ya mbunge na Naibu Waziri wa maji kuhusu hatua ya dharura iliyochukuliwa na serikali kuwapatia maji na kusitisha michango iliyojaa utata, maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano walikipuka kwa mayowe ya furaha na kumshangilia mbunge wao huku wengine wakiwapigia Makelele ya wezi wezi serikali ya kijiji.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni