Mkuu wa Jeshi la Burundi, ameahidi
utii kwa mamlaka ya nchi baada ya Waziri wa Ulinzi kutangaza kuwa
jeshi halitaunga mkono upande wowote kufuatia wiki moja ya ghasi za
maandamano ya kisiasa.
Mkuu huyo wa jeshi Jenerali Prime
Niyongabo amesema jeshi linabakia kuwa tiifu kwa jamhuri ya Burundi
na kuheshimu sheria na taratibu pamoja na watawala wa nchi.
Awali jumamosi taarifa ya Waziri wa
Ulinzi Jenerali Pontien Gaciyubwenge ilitangaza kuwa jeshi halitakuwa
na upande wowote na kutaka kusitishwa mashambulio ya raia ambayo
yanachochea mgawanyiko.
Taifa hilo dogo la Afrika ya Kati
limetumbukia katika maamndamano yaliyodumu kwa wiki moja baada ya
rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania urais kwa muhula wa
tatu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni