MKUU wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu Paul Mzindakaya (kushoto ) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Charles Lukale wakati akikabidhi moja ya Power Tiller kwa vikundi vinne vinavyojishughulisha na kilimo bora wilayani humo ili viweze kuondokana na umasikini kupitia katika sekta ya kilimo.
Na Shushu Joel,busega.
MKUU wa Wilaya ya Busega mkoani Simiyu Paul Mzindakaya amevikabidhi Power tTiller vikundi vinne vinavyojishughulisha na kilimo bora wilayani humo ili viweze kuondokana na umasikini kupitia katika sekta ya kilimo.
Akikabidhi Power Tiller hizo kabla ya kuanza kwa baraza la madiwani, Mzindakaya aliwataka wanavikundi wote waliokabidhiwa power tiller hizo kuweza kuzitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa na vikundi hivyo.
Aliongeza kuwa power tiller ni sawa na kuwa na tractor kwani zinafanya kazi nyingi sana mashambani na majumbani, cha msingi ni kuzitunza ili ziweze kudumu na pia kuwaletea maslahi makubwa kwenye vikundi vyenu alisema.
Aidha Mzindakaya alizibainisha baadhi ya kazi zinazofanywa na power tiller ni kulimia,kubebea mizigo,kubeba mbolea,kuchota michanga,maji na kokoto hivyo nawasihi mzitumie vile ipasavyo ili ziweze kuwaletea manufaa makubwa katika vikundi vyenu na mkizingatia hayo yote aminini mtaupiga vita umasukini, alisema.
Vikundi vilivyopewa power tiller hizo ni Igembesabo kilicho kijiji cha ngasamo,Nguvu kazi kilicho katika kijiji cha Ngasamo,Twiga kilicho katika kijiji cha Badugu na cha mwisho ni kikundi cha Mapambano kilicho katika kijiji cha Badugu na kuongeza kuwa power tiller hizo nne zimeghalimu kiasi cha shilingi 33,585,000.00 kupitia mpango wa DADPs.
Kwa Upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashaul hiyo Gaudencia Bamugileki alivipongeza vikundi hivyo kwa uvumilivu wao waliouonyesha kwani ni mda mrefu tangu watume maombi yao ya kusaidiwa kupewa kwa power tiller hizo na sasa wamekabidhiwa.
Bamugileki amewataka wanavikundi kuweza kuzitumia kwa ajili ya kazi stahiki ili ziweze kuleta tija kwao.
Sitta Gidion ni katibu wa kikundi cha Igembesabo anaipongeza serikali ya Tanzania kwa ujumla kwa kuweza kutambua umuhimu wa vikundi hasa viliovyoko vijijini.
Pia katibu huyo aliongeza kuwa msaada huu umefika wakati mwafaka hivyo wao kama Igembesabo watahakikisha wanazitumia kwa mahitaji stahiki katika vikundi vyao na hii ni kutokana na hali halisi ilivyo katika wilaya ya Busega .
Kwa upande wake mwakilishi wa kikundi cha Nguvu kazi Monika Mathias amempongeza mkuu wa wilaya na ofisi yake kwa ujumla kwani wao walikuwa wamesha kata tama na power tiller hizo ila sasa wamekabidhiwa.
Aliongeza kuwa furaha niliyonayo ni ile iliyozidi kifani na hii ni kutokana na pale mtu unapokuwa unahitaji kitu lakini kinachelewa kufika na mwisho wa siku unakipata hivyo furaha ni kubwa sana.
Na kwa upande wa matumizi yake wako vijana ambao tulikwisha waaandaa mapema kwa ajili ya kazi hii hivyo pia kikundi chetu kimeweza kutoa ajira kwa baadhi ya vijana na hata hivyo tutawatengenezea vijana wengine waweze kupata ajira kupitia kikundi chetu cha nguvu kazi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni