Mtuhumiwa wa wizi wa fedha za
mashine za (ATM), Annuar Ally, mwenye asili ya kiarabu, mkazi wa
Nairobi nchini Kenya, amekamatwa leo jijini Arusha na askari wa
kutuliza ghasia, baada ya kukutwa akijaribu kubomoa mashine ya ATM ya
benki ya Barclays tawi la Kituo cha mabasi.
Akizungumza na waaadishi wa habari
ofisini kwake, Afisa Mikopo wa tawi la benki hiyo, Regina Kitali
amesema wao waliingia ofisini kama kawaida ila wakiwa ndani majira
ya saa tano asubuhi, walisikia mlio usio wa kawaida kwenye mashine ya
ATM, wakalazimika kumtaarifu mlinzi wao nje.
Amesema mlinzi lipoingia ndani ya
chumba cha ATM, alimkuta mtuhumiwa huyo akiwa anataka kutoka, ila
mlinzi alijaribu kumuhoji, alijifanya anataka kutoa pesa ila mshine
haifanyi kazi na mlinzi alipoangalia mashine aliona mishumari yote
iliyofungwa mashine hiyo imefunguliwa na
hapo akalazimika kupiga kelele na
mtuhumiwa akakikmbia.
Regina amesema baada ya kukimbia
mtuhumiwa alilazimika kuingia benki ya NBC jirani na eneo hilo na
kutupa mashine maalum anayotumia kuibia fedha katika ATM na hapo
alikamtwa.
Regina amesema kikubwa pamoja
hajaiba fedha hizo, lakini wateja wachukue tahadhari kubwa wanapofika
katika mashine hizo na kukuta hali tofauti, watoe taarifa malka
husika.
Naye mmoja wa Mashuhuda wa tukio
hilo ambaye ni mfanyakazi wa benki ya NBC, ambaye hakutka kutajwa
jina lake, alisema sura ya mtuhumiwa huyo siyo ngeni, kwani
walishapewa taarifa zake kuwa anatafutwa na Polisi kwa kufanya
uhalifu maeneo mbalimbali.
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha,
Liberatus Sabasi, alipopigiwa simu ya kiganjani, kuhusiana na tukio
hilo, amekiri kuwa mtuhumiwa huyo kushikiliwa na jeshi la Polisi na
kusema kwa sasa hana maelezo ya kina kwa sababu bado anaendelea
kuhojiwa na wakimaliza mahojiano watapata cha kueleza wananchi.
Mwisho
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni