.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 19 Mei 2015

RAIS KIKWETE KATIKA DHIFA YA KITAIFA ALIYOMUANDALIA MGENI WAKE RAIS WA MSUMBIJI FILIPE NYUSI

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi katika dhifa ya kitaifa iliyofanyika jana usiku Ikulu jijini Dar es Salaam.
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akihutubia kwenye dhifa.
3
                                                         Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi akizungumza.
4
        Baadhi ya maafisa balozi waliohudhuria dhifa wakibadilishana mawazo.
5
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba akibadilishana mawazo na. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Julieth Kairuki.

6
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye na Mbunge wa Singida Mjini (CCM) Mohamed Dewji na Mfanyabiashara Maarufu nchini Yusuph Manji.
7
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu.
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya viongoz wa Serikali ya Msumbiji.
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba.
10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na Mnadhimu Mku wa Majeshi , Samuel Ndomba.
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (mwenye tai nyekundu) akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakifurahia burudani ya kikundi cha ngoma baada ya kumalizika kwa dhifa ya Kitaifa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, akumuongoza mgeni wake kutoka nje ya ukumbi wa Ikulu.
13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, akimuaga mgeni wake.
 

                                                                           Hussein Makame-MAELEZO

RAIS wa Msumbiji Filipe Nyusi amewaahidi raia wa nchi hiyo wanaoishi hapa nchini kuwa watapatiwa vitambulisho vya uraia baada ya kukamilisha utaratibu wa kuandaa vitambulisho hivyo.
 

Amesema hayo wakati alipokutana na kuzungumza na raia wa Msumbiji wanaoishi Tanzania kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi hapa nchini.
 

Alisema utaratibu huo unafanyika kwa raia wa Msumbiji wanaoishi nchi mbalimbali na kwamba ndani ya wiki mbili wanaweza kukamilisha utaratibu wa kupata vitambulisho hivyo.
 

Aliongeza kuwa katika mfululizo wa ziara zake za kikazi Rais Nyusi atakwenda nchini Afrika Kusini Jumatano ijayo ambapo atahakikisha raia wa Msumbiji wanaoishi nchini humo wanapata vitambulisho.
Kwa upande mwingine Rais Nyusi alisema kwa sasa hali halisi ya Msumbiji imetulia na wanapambana kuhakikisha amani inaendelea kuimarika nchini humo.
 

Katika mkutano huo raia wa Msumbiji walipata nafasi ya kutoa mchango wao na kuuliza maswali ambapo baadhi yao wamemshukuru Nyusi kwa kuichagua nchi ya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kuitembelea baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo.
 

Kwa upande wake, raia wa nchi hiyo Yasin Nomuya alimuomba Rais kuwawekea utaratibu raia wanaoishi nchi za nje na kupata ujuzi, kurudi nchini kwao ili kutoa mchango wa kuijenga Msumbiji.
 

Akijibu swali hilo Rais Nyusi aliwataka raia wa Msumbiji waliopo nje ya nchi hiyo kwenda kwenye balozi za nchi husika ili waweze kufamahamishwa ni njia gani wanaweza kuzitumia ili kuijenga nchi yao.
 

Aidha aliwaomba raia hao wa Msumbiji kushirikiana na wananchi wa Tanzania katika kupata huduma mbalimbali zinazotolewa nchini ikiwemo huduma za afya.
 

Raia hao wa Msumbiji wanaoishi hapa nchi walimpa zawadi mbalimbali Rais Nyusi na mkewe kama ishara ya kuonesha upendo wao kwake na kumtakia mafanikio katika kipindi chake cha uongozi.
 

Rais Nyusi ameondoka mchana wa leo kuelekea Zanzibar ambapo anatarajiwa kukutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na kuzungumza na raia wa Msumbiji wanaoishi visiwani humo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni